Jinsi ya kupata kazi nzuri kwa haraka – How to get a good Job

March 2, 2017 by Stuffzoom

Filed under Jobs, Jobs in Tanzania

Last modified March 2, 2017

Tambua njia za kupata kazi kwa haraka

 • Tengeneza network nzuri, Kuwa na mawasiliano na ndugu na marafiki walio makazini tayari, ili kukupasha habari kuhusu nafasi za kazi haswa zile zinazo tangazwa ndani, kwani baadhi ya makampuni hutangaza nafasi za kazi ndani (internally) kwa wafanyazi.
 • Fanya interviews nyingi kadri uwezavyo, kwani zitakujenga na kukupa ujasiri zaidi

Jinsi ya kufanikiwa kwenye Interviews

 • Usijishushe – Wengi hujishusha sana hadi kusahau dhamani yao, kwakudhani kwamba ndio wataonekana wanyenyekevu na kuaminika. Onyesha msimamo na kujiamini, hakuna mwajiri anayetaka mtu asiyejiamini
 • Uliza maswali, Usisubiri tu wewe uulizwe. Ila uliza maswali yenye tija na yatakayo kuwa changamoto kwao
 • Mtazame anaye kuuliza swali, epuka kupepesa macho wakati wa interviews, hii inaonyesha kutojiamini
 • Epuka Maelezo mengi, Usijielezee sana, kwani wakati mwengine kwenye maelezo yako ndiko maswali yanapotoka.
 • Mwisho wa interview waambie kuwa umefurahi na washukuru kwakukupa nafasi ya interview, pia waeleze endapo watakupa nafasi utafanya nini

Ukiweza kufanya hayo, huwezi kukosa kazi. Nakutakia kila la heri

By, Stuffzoom – Ajira Mpya Tanzania

Related Articles

         Leave a Comment

         Google+ Twitter Facebook